Jumapili , 15th Sep , 2019

Choo cha Dhahabu kilichoundwa kwa Karati 18 chenye thamani ya zaidi Shilingi Bilioni 11.5 kimeibiwa, katika jumba la Bleinheim huko nchini Uingereza usiku wa kuamkia leo.

Choo hicho kilikuwa kikitumika kwa ajili ya maonesho na kumilikiwa na msanii Maurizio Cattelan, ambaye ni raia wa Italia, ambapo watu mbalimbali walikuwa wakitembelea na kulipia pesa ili ya kukitumia.

Kuibiwa kwa choo inaelezwa kuwa iligundulika hasa baada ya maji kuanza kutapakaa ndani ya jumba hilo, kutokana na kuondolewa kwa nguvu katika eneo ambapo kilikuwa kimewekwa na kuunganishwa na mifumo ya maji, kama choo cha kawaida kinavyokuwa.

Mpaka sasa mtu mmoja anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano, huku jumba hilo likifungwa kwa muda kwa ajili ya uchunguzi zaidi na Polisi.

Chanzo: BBC