Jumamosi , 21st Feb , 2015

Wajasiriamali Vijana katika soko la Ilala jijini Dar es Salaam nchini Tanzania wameitaka serikali kuwasaidia katika upatikanaji wa mitaji kutokana na sasa mikopo mingi wanayochukua kurudisha kwa riba kubwa na huchukua muda mrefu hadi kuipata.

Wakizungumza na EATV jijini Dar es Salaam, wajasiriamali hao Vijana wamesema kwa sasa wamekuwa wakikosa msaada wa upatikanaji wa mitaji ikiwemo mikopo kutoka serikalini jambo ambalo wengi wao kushindwa kuendesha biashara zao.

Vijana hao wajasiriamali pia wameitupia lawama serikali kwa kutishia kuwaondoa mara kwa mara katika eneo hilo na hivyo kusababisha kukata tamaa ya kazi wanazofanya.

Wamesema mara kadhaa serikali imekuwa ikitoa matamko ya kutaka kuwaondoa huku wakifahamu kwamba hawana maeneo mengine ya kwenda jambo ambalo wamesema kuna haja ya kufikiriwa na serikali na kuwasaidia badala ya kuwapa vitisho vya mara kwa mara vya kutaka kuwaondoa.