Afisa vipimo akikagua kuona iwapo mtungi wa gesi una ujazo unaostahili
Kutokana na hali hiyo, wakala huo umesema utaendelea kufanya ukaguzi wa kushtukiza kwenye maeneo yote inakouzwa gesi nchini kwa lengo la kubaini wanaojihusisha na udanganyifu huo.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo Dkt. Ludovick Manege amesema hayo jijini Dar es Salaam na kufafanua kuwa udanganyifu unaofanywa katika biashara ya gesi unatumia mbinu na utaalam mkubwa ambao wakala hiyo ina wajibu wa kuubaini kwa lengo la kuwalinda wateja na watumiaji wa gesi.
Kwa mujibu wa Dkt. Manege, tayari ipo sera na sheria inayoelekeza wajibu wa wakala hiyo katika kuwalinda wateja na kueleza jinsi watakavyotimiza wajibu wa kuwalinda wateja kuwa ni pamoja na kukagua mizani ya kupimia gesi, kuona iwapo mitungi ya gesi inayouzwa imefuata taratibu na maelekezo ya kitaalam kuhusu ujazo.