Jumanne , 19th Mar , 2024

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikiliwa watu kumi kwa tuhuma za kutorosha kilo 9.5 za madini ya dhahabu.

Waziri wa madini Anthony Mavunde amesema thamani ya dhahabu iliyokamatwa ina thamani ya shilingi bilioni 1.5 ambapo watuhumiwa hao walikamatwa katika eneo la Ilomba Jijini Mbeya.

Mavunde amesema tukio hili ni la pili kutokea mkoani Mbeya na kuagiza Kamishna wa madini kuzifuta leseni zote zinazomilikwa na watu hao pamoja na leseni zote zinazomilikiwa na watu hao nje ya Mkoa wa Mbeya 

Watu hao wamekamatwa wakiwa na vifaa vya kuchomea dhahabu na mizani ya kupimia pamoja na dawa za kusafishia ambapo uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani