Jumatatu , 28th Apr , 2014

Wakazi wa Bunda Mkoani Mara wametakiwa kutouza chakula na wajiwekee akiba ili kukabiliana na hali ya njaa inayoanza kujitokeza kwenye Baadhi ya wilaya za Mkoa huo kwa sasa na kuathiri maisha yao.

Mahindi ni moja ya vyakula vinavyotegemewa sana na wakazi wa wilaya ya Bunda

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Mbunge wa Viti maalum Vijana Mh. Ester Bulaya wakati akiongea na East Africa Radio kuhusu hali ya njaa iliyoanza kujitokeza katika Sehemu Mbalimbali za mkoa wa Mara na jitihada za kukabili tatizo hilo.

Mhe.Bulaya amesema kwa sasa hali ya chakula katika wilaya ya Bunda ni nzuri lakini itaweza kuwa mbaya endapo wananchi hawatahifadhi chakula ili kukabiliana na njaa wakati wa ukame.