Ijumaa , 2nd Apr , 2021

Wananchi wa Kenya wanaoishi katika mipaka ya Kenya na Tanzania wameahidi  kuendelea kwenda kanisani upande wa Tanzania iwapo Serikali ya Kenya haitaondoa marufuku ya kuingia katika maeneo ya ibada.

Picha Ikulu ya Kenya

Wiki moja baada ya rais wa Uhuru Kenyatta Kenya kuweka masharti mapya kukabili maambukizi ya corona, masharti hayo yakizuia watu katika maeneo ya burudani na ya ibada, Wakenya eneo la Namanga kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania wanasema kuwa maisha yataendelea na wamekuwa wakihudhuria ibada katika taifa jirani, na kumuomba rais wao kuondoa vikwazo alivyoweka.

Wanasema serikali huenda ikasababisha madhara makubwa kwa kuwazuia watu katika maeneo ya ibada, wakisema kuwa kipindi hiki ambacho wanafunzi wapo nyumbani kwa likizo, ni muhimu wawe kanisani kwa mafunzo na maelekezo.

Hapo jana Rais Uhuru Kenyatta aliitetea hatua yake ya kufunga nyumba za ibada na kuongeza masharti, akisema haya yote ni kwa ajili ya kuwalinda wananchi na kuwataka wawe wavumilivu.