Jumatano , 17th Dec , 2025

Wakili Peter Madeleka amefungua rufaa akihoji misingi ya kisheria iliyotumiwa na Mahakama Kuu katika kuamua shauri hilo, ikiwemo tafsiri ya mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufuta sherehe za maadhimisho ya Uhuru.

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma imetupilia mbali shauri la kupinga kufutwa kwa Sherehe za Uhuru 2025 lililofunguliwa na Wakili Peter Madeleka leo Disemba 17, 2025.

Kufutia uamuzi huo wa Mahakama Wakili Peter Madeleka amefungua rufaa akihoji misingi ya kisheria iliyotumiwa na Mahakama Kuu katika kuamua shauri hilo, ikiwemo tafsiri ya mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufuta sherehe za maadhimisho ya Uhuru.

Awali, Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma ilitupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Wakili Madeleka dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akipinga uamuzi wa kufuta Sherehe za Uhuru zilizopangwa kufanyika mwaka 2025.

Katika shauri la awali, Wakili Madeleka alidai kuwa uamuzi wa kufuta sherehe hizo ulikuwa kinyume cha misingi ya Katiba na utawala wa sheria kabla ya Mahakama kuamua kuwa shauri hilo halina msingi wa kisheria.

Kufuatia rufaa ya Wakili Madeleka, suala hilo linatarajiwa kupelekwa mbele ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kwa hatua zaidi za kisheria.