
Inaelezwa kuwa wafugaji walimpiga mkulima mmoja na kumuua na kisha wakulima wakachukua sheria mkononi ya kuwaua wafugaji watatu. Tukio hilo limetokea Novemba 8/2022
Kamishina wa Operesheni na Mafunzo wa jeshi la Polisi Tanzania CP Awadhi Haji amesema jeshi la polisi pamoja na serikali hawakubali kitendo cha watu wachache kujichukulia sheria mikononi na kutekeleza mauaji
Katika kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji mkuu wa mkoa wa Ruvuma kanali Laban Thomasi amesema mkoa wa Ruvuma umetenga vitalu kwa ajili ya wafugaji hivyo ameagiza wafugaji wote wapelekwe kwenye vitalu ambavyo vimetengwa na serikali
Wakielezea chanzo cha mauaji hayo Sophia Hashimu ambaye ni mke wa mkulima aliye uawa na wafugaji pamoja na Juma Chowo kaka wa mkulima aliye uawa wamesema wafugaji walifika kwenye shamba la nyanya la marehemu na kulishia ng'ombe mazao ambayo yalikuwepo kwenye shamba na marehemu alipo wafukuza ng'ombe hao ndipo wafugaji walipo muambia ataona na asubuhi mkulima huyo akakutwa ameuawa.