Jumamosi , 21st Mar , 2020

Wakazi wa kijiji cha Ruaha Mbuyuni katika Kata ya Ruaha, Mbuyuni wilayani Kilolo wanakabiliwa na tatizo la usafiri kutokana na kuharibika kwa baadhi ya barabara katika eneo hilo kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi sasa.

Kamati ya Ulinzi na Usalama wakiwa katika Ukaguzimradi wa Barabara iliyoharibika

Baadhi ya watumiaji wa njia hiyo wamesema imekuwa na athari kubwa katika uchumi wao maana wakazi wengi kijijini hapo ni wakulima wa nyanya na vitunguu.

Wakiongea wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya hiyo kwa lengo la kugagua miundombinu ya barabara, wananchi hao wamesema wamekuwa na wakati mgumu kusafiri kutokana na baadhi ya barabara kuharibiwa vibaya.

Akizungumza mara baada ya kukagua miundombinu hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asiah Abdalah amesema wananchi wasiwe na shaka tatizo hilo litashughulikiwa.