Alhamisi , 16th Feb , 2023

Zaidi ya wanafunzi 600 wa shule ya sekondari Msimbu, Kisarawe mkoani Pwani, wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa taulo za kike kutokana na familia zao kushindwa kuwanunulia hali inayowalazimu walimu kuingia mifukoni au kuwapatia akiba walizonazo ili kuwanusuru wanafunzi wao.

Wanafunzi 600 wa shule ya sekondari Msimbu

Wanafunzi wamesema hali duni ya kimaisha katika familia wanazotoka ikilinganishwa na uhitaji wa taulo za kike pindi wanapokua katika hedhi imepeleka wanafunzi wengi wa kike kuomba msaada kwa walimu wao na wanapokosa kabisa huamua kurudi nyumbani ili kuondokana na aibu.

Akielezea jitihada wanazochukua pindi wanafunzi wanapokua katika hali hiyo mwalimu wa malezi shuleni hapo amesema hulazimika kutoa fedha mfukoni au huwapatia akiba walizonazo kwaajili ya kuwalinda na kadhia hiyo.

Kufuatia changampoto zinazowakabili wanafunzi kipindi cha hedhi mkuu wa wilaya ya Kisarawe Fatma Nyangasa, anaelezea mkakati wa serikali wa kuhakikisha kila inapojengwa miundombinu mipya inakua na chumba maalum kwa ajili ya kuwastiri watoto wa kike wanapokua katika hedhi.