Jumatatu , 15th Aug , 2022

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amuagizla Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji nchini Dkt Anna Makakala kuwachukulia hatua maafisa uhamiaji wa Zanzibar na Dar es salaam waliohusika kuchukua rushwa kwa wageni wakati wa utoaji wa vibali

 

Rais pia ameagiza wale wote waliohusika na upotevu wa fedha hizo hususani katika vituo vya Zanzibar na Daresalaam washughulikiwe ili kutoa taswira kwa anayekosea ndani ya jeshi kuwa anashughulikiwa ili hao wanajiofunza wasiige jambo hilo na wajue afisa anayekosea anachukuliwa hatua za kinidhamu. 

Lakini pia Rais amelitaka Jeshi la uhamiaji Nchini kuondoa na kupunguza urasimu wa utoaji wa vibali kwa wageni na wanyeji wanaoingia na kutoka hapa nchini badala yake kuharakisha utoaji wa vibali hivyo hali ambayo imekuwa ikilalamikiwa kwa kipindi kirefu

Rais Samia alitoa maagizo hayo Mkoani Tanga wakati akifunga Mafunzo ya awali ya Jeshi la uhamiaji kwa maafisa 818 yaliyopewa jina la oparesheni ujenzi katika chuo cha uhamiaji cha Boma - Kichakamiba kilichopo wilayani Mkinga Mkoani Tanga. 

Rais Samia alisema katika vituo wanashuhudia vitendo vya upokeaji wa rushwa pamoja na unyanyasaji kwa wageni wanaoingia na malalamiko kutoka kwa wageni na kueleza kuwa maafisa hao ni wale walioko kwenye vituo ambao pengine hawakupitia vyuoni na kuagiza maafisa hao warudi vyuoni na wale waliopita vyuoni wapelekwe maofisini wakafanye kazi kwa kuwa tayari wameshakuwa wazalendo na nchi yao. 

"Kauli mbiu hii ya umoja, upendo, uwajibikaji,  mshikamano na kukataa rushwa ninawataka muishi kwa vitendo nimeipenda sana kauli mbiu yenu, "Alisema Rais Samia. 

Aliongeza kuwa lakini pia nimesikia kuna maafisa askari ambao sio  waaminifu kuna kesi kwenye mafaili sasa hivi fedha zinazotolewa za Visa na Vibali wanazigeuza za kwao na wanaweka mifukoni,  katika utafiti mdogo uliofanywa mapema mwaka huu hasa pale vituo vya Zanzibar na Dar es salaam nimegundua upotevu mkubwa wa fedha na Visa ambao unafanywa na maafisa wa uhamiaji kwa vitendo vya aina hii viende vikakomeshwe ndani ya jeshi hili na turudi kwenye maadili ya jeshi kama wimbo wetu mliokuwa mkiimba hapa, "alisema Rais