Jumanne , 22nd Nov , 2022

Taaifa mpya zinasema kwambatetemeko la ardhi katika kisiwa kikuu cha Indonesia cha Java limesababisha vifo vya mamia ya watu huku mamia wengine wakijeruhiwa.

 

Tetemeko hilo  mji wa Cianjur magharibi mwa Java, katika kina kifupi cha kilomita 10 swa na maili 6 kulingana na takwimu za Utafiti wa Jiolojia wa Marekani.

Watu kadhaa walipelekwa hospitalini, huku wengi wakitibiwa nje.

Waokoaji wamefanya kazi usiku kucha kujaribu kuwaokoa wengine wanaodhaniwa kuwa bado wamekwama chini ya majengo yaliyoporomoka.

Eneo ambalo tetemeko hilo lilitokea lina watu wengi na linakabiliwa na maporomoko ya ardhi, huku nyumba zilizojengwa zikiwa ni za viwango vya chini.

Idadi kamili ya watu waliouawa kufikia sasa bado haijulikani. Shirika la Kitaifa la Kukabiliana na Majanga nchini Indonesia BNPB limesema idadi yao rasmi ya vifo ni 103, na kuongeza kuwa idadi nyingine iliyotolewa na gavana wa mkoa huo Ridwan Kamil .

BNPB imesema watu wengine 390 wamejeruhiwa na kwamba watu 7,000 wamejihifadhi katika maeneo mbalimbali katika eneo hilo.