Ijumaa , 27th Aug , 2021

Kampuni ya Samsung imeweka zuio kwa TV zote za kisasa zilizoibiwa Afrika Kusini wakati wa ghasia za uporaji na maandamano yaliyofanyika mwezi Julai mwaka huu, na kuzifanya zisiweze kufanya kazi tena.

Runinga

Mfumo huo wa kuzima runinga zote zilizoibwa wakati wa maandamano hayo umeangalia orodha ya namba za usajili kabla ya kuzuia matumizi yake na kwamba TV hizo zinaweza kufanya kazi endapo aliyeiiba anatumia mawasiliano ya intanent kinyume cha sheria.

Afrika Kusini ilikuwa na maandamano ya ghasia mwezi Julai hali iliyopelekea baadhi ya makazi ya watu na maduka makubwa kubomolewa na watu kuiba vitu, maandamano ambayo yalidaiwa kuchochewa na tataizo la ajira nchini humo ambapo zaidi ya watu 300 waliuawa.

Chanzo BBC Swahili