Alhamisi , 12th Mei , 2016

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki imewataka waandishi wa habari nchini kushiriki kwenye Mkutano wa Vyombo vya Habari utakao ambatana na tuzo maalumu uliondaliwa na Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa imewataka waaandishi wa habari nchini kushiriki kwenye Mkutano wa Vyombo vya Habari utakao ambatana na tuzo maalumu uliondaliwa na Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,B araza la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na wanachama wa Jumuia hiyo kwa lengo lakupanua wigo wa habari kimataifa na kutambua mchango wa waandishi wa habari.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Robi Bwiru amesema mkutano huo niwa 8 wa kilele wa wanahabari wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC-EABC MEDIA SUMMIT) ambao utafanyikia Nairobi Kenya utawasaidia waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari nchi kuongeza wigo wakupata habari ambazo zimekua ni ngumu kuzifikia na kuzipata kwa wakati sambamba na hilo waandishi watakaofanya vizuri zaidi watapata fursa yakujifunza shughuli zinazofanywa na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Amesema mkutano huo utajadili masuala mbalimbali yanayohusu tasnia ya habari na wadau mbalimbali,vile vile katika mkutano huo zitatolewa tuzo katika maeneo mbalimbali yanayozungumzia shughuli mbalimbali za mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wizara imetoa rai kwa waandishi wa Tanzania kutumia fursa hii na na kupeleka kazi zao ili kuweza kushiriki katika tuzo hizo na ushiriki katika tuzo hizo si tu utawapa ushindi wa tuzo bali pia utawatambulisha katika soko la ajira katika tasnia ya habari ndani na nje ya Jumuiya hiyo.