Alhamisi , 21st Mei , 2015

Jeshi la polisi mkoani Iringa limelazimika kutumia nguvu kuwatawanya wanafunzi wa chuo kikuu cha Rucu baada ya kutaka kufanya maandamano na kusababisha vurugu chuoni hapo.

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani A. Mungi akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao Makuu ya Jeshi la Polisi Iringa.

Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi ameeleza kuwa wanafunzi hao walitaka kufanya maandamano hayo kwa madai kuwa wamecheleweshewa mikopo yao.

Kamanda amesema kuwa wamewadhibiti makusudi wachuo hao ili wasitoke nje ya geti la chuo kutokana na kuhofia kuvuruga amani .

Aidha kamanda ameeleza kuwa jeshi la polisi linawashikilia wanafunzi 89 na kusema kuwa kwa yoyote atakayejaribu kuvunja amani ni lazimawatamchukulia hatua kali za kisheria bila kujari chochote.

Hata hivyo wakizungumza wanachuo hao wamesema kuwa kucheleweshwa kwa mikopo hiyo kunachangia maisha yao kuwa magumu.

Wakati huo huo Jeshi la hilo linawashikilia viongozi watatu wa waendesha pikipiki kwa tuhuma za kuwafanyia fujo maafisa watatu wa mamlaka ya usafirishaji wanchi kavu na majini Sumatra.

Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi amesema kuwa maafisa hao wamefanyiwa fujo wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya kawaida katika eneo la chuo cha mkwawa manispaa ya Iringa.

Kamanda amesema kuwa jeshi la polisi tayari limeshafungua jalada na watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani muda wowote yatakapoletwa mashtaka.

Aidha kamanda amesema kuwa endapo matukio kama hayo hayata kemewa mapema yatachangia uvunjifu wa amani hivyo amewataka wananchi pamoja na wanahabari kushirikiana kwa pamoja katika kukemea masuala hayo.

Hata hivyo akizungumza afisa mfawidhi wa mamlaka ya usafirishaji wa nchi kavu na majini Sumatra mkoa wa iringa Bartel Patel amekiri kufanyiwa kwa kitendo hicho.