Jumanne , 26th Jul , 2022

Kwa mujibu wa Mkuu wa shule ya King David, iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani Daniel Msilu, amesema wanafunzi wa shule yake waliofariki ni watano pamoja na dereva, na kusema wanafunzi wengine watatu pamoja na mwanamke mmoja walikuwa wamepewa lifti.

Gari la basi lililopata ajali

Ajali hiyo imetokea hii leo Julai 26, 2022, wakati watoto hao wakitolewa majumbani kupelekwa shuleni na ajali hiyo imetokea  baada ya breki ya gari la shule kufeli wakati likiteremka kwenye mlima katika eneo la Mjimwema.

Watoto waliojeruhiwa katika ajali hiyo wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya mkoa wa Mtwara ya Ligula.