Jumatano , 5th Oct , 2022

Kufuatia Mji wa Njombe kuwa na mwingiloano mkubwa wa wageni kutoka ndani na nje ya nchi kibiashara, Serikali kupitia idara ya afya imelazimika kuchukua tahadhali madhubuti dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa ebola kwa kuanza kutoa elimu kwa wananchi majumbani na katika mikusanyiko

Tanzania ni mshirika wa jirani na Uganda ambayo hadi sasa imeripotiwa na mikasa ya zaidi ya 44 ya wagonjwa wa Ebola huku vifo vikifika 23 jambo linaloisukuma serikali kuanza kuchukua hatua za kujikinga.

Katika kukabiliana na tishio la ugonjwa wa Ebola, Baraza la halmashauri ya mji wa Njombe linalazimika kumwita mtaalamu wa tiba katika vikae vyake ili kuendelea kuelimisha viongozi wa siasa ili wakatumie nafasi yao kuelimisha umma juu ya ugonjwa huo.

Awali akitoa elimu kwa watumishi na viongozi wa siasa hususani madiwani Dr Isaya Mvinge ambaye ni mratibu wa tiba halmashauri ya mji wa Njombe anaeleza visababishi,dalili na namna ya kujikinga na maradhi hayo.

Wakizungumzia manufaa ya elimu walitopatiwa juu ya ugonjwa wa ebora baadhi ya madiwani akiwemo Erasto Mpete na Tumaini Mtewa wanasema imekuja katika wakati muafaka na kwamba wanakwenda kuchukua hatua ya kuelimisha umma ili kunusuru maambukizi kutoka wageni.

Katika hatua nyingine baraza la madiwani limepokea wageni kutoka serikali ya ujerumani ambao wameingia mashirikiano na halmashauri ya mji wa Njombe katika utekelezaji mradi wa utunzaji wa mazingira utakaohusisha ujenzi wa vizimba na nishati ya umeme wa upepo na elimu wenye thamani ya zaidi bil 4.Kama ambavyo Sebastian Randig mmeneja mazingira wilaya ya Miltenberg na Emmanuel George katibu tawala Njombe anavyoeleza.