Jumatatu , 8th Feb , 2016

Wananchi wa wilaya ya Tarime mkoani Mara wamelalamikia tabia za baadhi ya askari wa jeshi la polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya kuwabambikizia kesi za mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama, ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Tarime , Glorious Luoga

Wananchi hao wa wametoa malalamiko yao mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na Mwenyekiti wake Bw. Glorious Luoga wakati wakisikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa wilaya hiyo pamoja na kuelezea mipango mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano.

Wananchi hao wamesema kuwa ubambikiwaji kesi huo unatokana na kuwepo kwa mianya ya rushwa kutoka kwa askari hao wanaowakamata huku wakiongeza kwa kusema keshi za kawaida zinachukuliwa muda mrefu mpaka kuja kutolewa maamuzi kitendo ambacho wamesema kimesabisha wananchi wengi wasio na uwezo wa fedha kwa ajili ya kutoa rushwa kuzekea magerezani.

Akijibu malalamiko hayo Mwenyekiti huyo wa kamati ya ulinzi na usalama, ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Tarime, pamoja na kutoa ahadi ya kukomesha vitendo hivyo , ametumia nafasi hiyo kuruhusu vikundi vya ulinzi shirikishi maarufu kama Seiga kwa masharti ya kutokiuka katiba ya nchi, sheria na haki za binadam.