
Mongella ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama amesema hayo leo June 11 2022 katika tarafa ya loliondo wilaya ya Ngorongoro alipokuwa anaongea na vyombo vya habari kuhusiana na zoezi linaloendea la uwekaji mipaka katika wilaya hiyo.
Amewambia waandishi wa habari kuwa kuna baadhi ya watu na mitaandao ya kijamii kupotosha kuhusiana na kinachoendelea katika zoezi la uwekaji mipaka katika wilaya ya Ngorongoro.
Aidha amesema kuwa katika siku ya jana kulitokea kundi la watu wenye silaha ambapo askari mmoja alijeruhiwa na kukimbizwa hosptal lakini alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu.