Jumatatu , 13th Jan , 2020

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro, amewataka wakulima wa Korosho ambao tayari wamekwishapata malipo yao, wawekeze fedha zao kwenye mambo ya msingi na si kutumia kwa ajili ya kufanya sherehe.

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro

Mtatiro ametoa kauli hiyo wakati wa hitimisho la mnada wa 9 wa zao la  Korosho, ambapo amesema wananchi wa Tunduru, kupitia mnada huo wamepata zaidi ya bilioni 60.

"Tunavyozungumza hapa Mheshimiwa Waziri, wananchi wa Tunduru wamepata zaidi ya Bilioni 60 za Korosho, 2018 walipata bilioni 61 katika kipindi cha miezi 2 mpaka 3, niwasisitize wananchi muwekeze fedha hizi kwenye mambo ya msingi." amesema Mtatiro.

"Sasa hivi kila ninapopita wananchi ni sherehe, wananchi wanakula maisha, kila nyumba ukipita vitenge na Kanga vimefungwa nje yaani sherehe kwa sherehe " ameongeza Mtatiro.