Ijumaa , 18th Sep , 2020

Mkuu wa wilaya ya Temeke Godwin Gondwe, amesema aneo la One stop jawabu huko Mbagala zakhiem limekuwa na mafanikio kwa wananchi kutatuliwa changamoto zao kwa haraka tofauti na hapo awali.

Mkuu wa wilaya ya Temeke Godwin Gondwe.

Akiongea na EATV leo, Gondwe amesema wananchi wamekuwa wakikabiliwa na matatizo mengi lakini walikuwa wanashindwa kupata huduma kwa karibu lakini kwa  kipitia utoaji wa huduma hizo wameweza kutatua changamoto zao.

Kwa  upande wao wananchi wanaopata huduma katika eneo hilo la one stop jawabu wameeleza namna walivyonufaika na huduma hizo ikiwemo upimaji wa magonjwa kama ya saratani