Jumamosi , 20th Apr , 2019

Wananchi wa Kijiji cha Igombola Kata ya Lupembe wilayani Njombe wamesema hawana Imani na Mwenyekiti wao wa kijiji aliyejulikana kw ajina la Josephati Kiluka kutokana na kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo na kudai kuwa anafanya kazi kwa maslahi yake binafsi.

Wakizungumza kwa wakati tofauti wananchi hao wamesema hawana imani na mwenyekiti huyo kwa kubadili mahali ambapo miradi ya maendeleo na kuyapeleka sehemu ambayo ni tofauti na makubaliano ya wananchi.

Wananchi hao wameeleza kuwa licha ya kubadili miradi ya maendeleo na kuielekeza tofauti wamesema pia amehujumu miradi ya maji katika kijiji hicho na bado imekuwa na changamoto kutokana na usimamizi mbovu wa kiongozi huyo.

Akijibu madai hayo Mwenyekiti Josephati Kiluka amedai kuwa taarifa zilizotolewa na wananchi hao kuwa hazina ukweli, na kusema miradi hiyo imeshindwa kukamilika kwa wakati kutokana na baadhi ya viongozi kuweka siasa kwenye miradi hiyo.

"Tatizo kubwa wanasiasa kwa sababu huwa wanaongea kuwafahadaa wananchi, lakini miradi mingi ya maendeleo imekwamba kutokana kuwekwa siasa, lakini hayo madai wanayotoa dhidi yangu si kweli." amesema mwenyekiti huyo Josephati  Kiluka