
Wakizungumza kwa masikitiko makubwa mbele ya Mbunge wa Jimbo la Igalula, baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wamesema kuwa ukosefu wa barabara imekuwa ni kero kubwa kwao inayosababisha hadi akina mama wajawazito kujifungulia njiani.
Akijibu kero hiyo, Mbunge wa jimbo la Igalula, Musa Ntimizi amewatoa hofu wananchi hao akisema tayari serikali imeshaitambua barabara hiyo ili kuanza kutengenezwa pindi bajeti itakapokuwa tayari.
Pia wakazi wa kijiji hicho wamesema licha ya kijiji chao kuitwa Vumilia lakini kwa sasa uzalendo umewashinda kwani wamevumilia mengi toka kijiji kianze mpaka leo hakuna barabara bora hali inayowafanya wabaki kama vile wako kisiwani hasa katika kipindi hiki cha mvua za masika.