
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba
Kauli hiyo ameita hii leo Agosti 20, 2021, Jijini Dar es Salaam, na kusema kwamba licha ya wananchi kutoa malalamiko juu ya ongezeko hilo lakini bado wameendelea kufanya miamala ya kutuma ama kupokea pesa na serikali tayari imekusanya kiasi cha shilingi bilioni 48.4 kutokana na tozo hizo, na kwamba mara baada ya majadiliano ya pande zote mbili serikali itakuja na tamko rasmi.
"Tuwaombe wananchi waendelee kuwa wavumilivu tujipe muda tu-engage na wenzetu kwamba, tulivyojumlisha kwetu na nyie huu mzigo umekuwa mkubwa sana kwa wananchi hivi kweli hatuwezi kuangalia nani apunguze wapi, kuna maeneo serikali imeenda kukutana juu kwa juu na watoa huduma na hii si kwa watu wa chini ni kwa watu wanaotuma miamala ya laki 8 au milioni 2," amesema Waziri Nchemba.
Aidha, awali akizungumza, Dkt. Nchemba amesisitiza kwamba suala la tozo za miamala limekuja kwa lengo la kuboresha huduma za wananchi, "Ombi langu moja kwa Watanzania wanaonitizama kwamba jambo hili ni letu sote sio la serikali, nchi hii ni yako wewe hapo ulipo na pesa ni yako na haya mambo tuliyokuwa tunapangilia tuyafanye ni yako, hivyo haya yote ni yetu".