Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini , IGP Simon Sirro
IGP Sirro amesema hayo wakati alipofanya ukaguzi wa ghafla kwenye kituo cha polisi Stakishari, Tabata Shule na Kawe jijini Dar es salaam, na kuwataka wenyeviti wa serikali za mitaa, watendaji kata na polisi kata kuendelea kuhamasish vikundi vya ulinzi shiurikishi ili kuhakikisha matukio ya uhalifu yanapungua kwenye maeneo yao.
Aidha, IGP Sirro amewataka madereva hasa wa pikipiki maarufu bodaboda kufuata masharti ya leseni zao na kuacha kujiingiza kwenye matukio ya uhalifu wa kutumia nguvu.


