
Mbunge huyo ametoa kauli hiyo Bungeni wakati akichangia mjadala wa bajeti 2022/23 ambapo amesema kauli hizo zinaweza kujenga matabaka na kufanya watu wa maeneo mengine nao kugoma kuhama kupisha miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali
"Kuna wanaosema kwamba wananchi wa Ngorongoro kuwahamisha eneo lile ni makosa kwa sababu wameshayazoea, tunatengeneza Double standard ya hali ya juu sana katika taifa letu, kwa sababu kama hili likisikilizwa maeneo mengine wakihamishwa kupisha miradi ya maendeleo watakataa" amesema Kishoa
Aidha Mbunge huyo amesema kumekuwa na baadhi ya watu wanaopotosha zoezi la kuwaamisha baadhi ya wakazi wa Ngorongoro huku akisema baadhi ni wanasiasa wanaotumia jambo hilo kitafuta 'Kiki'
"Wapo watu wanaaminishwa kwamba eneo hili kuna sjui mwarabu anataka kulichukua yani kuna propaganda za hovyo watu wanatafuta kiki, wanasiasa wanatafuta kiki, najiskia vibaya kwamba nipo kwenye nchi ambayo kuna mwananchi yupo nchi nyingine anamtukana Rais wa Tanzania"
Katika hatua nyingine mbunge huyo amesema anatamani na yeye angekuwa miongoni mwa wananchi wanaiohamishwa Ngorongoro kwa kuwa serikali imewatendea haki kwa kuwapa huduma zote za msingi na bora
"Leo wananchi wanahamishwa, unapelekwa eneo unajengewa nyumba, unakuta hospitali, shule, unapewa hati kama una wake watatu unapewa hati ya nyumba tatu, mimi naomba leo nitangaze rasmi naitwa Ole Kishoa ili nipelekwe kule na mimi nikapewe nyumba ya bure kabisa"