
Mkuu wa wilaya ya Ludewa, Andrew Tsere
Mkuu wa wilaya hiyo Andrew Tsere amesema baada ya kufika katika wilaya hiyo alibaini wanafunzi kukutana na changamoto nyingi ikiwemo ya mimba na uhaba wa walimu na kisha kuja na mpango wa elimu ya makambi na katazo la wanaume kusimama na wanafunzi katika mazingira yasiyo rafiki.
Hayo ameyabainisha kwenye kikao cha mapitio ya tathimini ya utekelezaji wa shughuli za uboreshaji na usimamizi wa elimu mkoa kilichohudhuliwa na Naibu Waziri wa TAMISEMI Dkt. Festo Dugange.
Wakati wilaya ya Ludewa ikiweka mkakati huo na kisha kuinua ufaulu kutoka asilimia 60 hadi 80 katika kipindi cha miaka mitatu, serikali ya mkoa wa Njombe kupitia kwa Katibu Tawala Judica Omary, imesema tatizo la upungufu wa walimu na mdondoko wa wanafunzi limekuwa kubwa hatua ambayo inamsukuma mkuu wa mkoa huo Anthony Mtaka kuweka msimamo mpya.