Jumatano , 2nd Mar , 2022

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Mawahanga, ametoa wito kwa wanawake nchini kushirikiana na kusaidiana katika kuwainua wanawake wanzao.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Mawahanga

Mhe. Janeth ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya #MwanamkeKinara ya East Africa Television na East Africa Radio, yenye lengo la kutambua mchango wa wanawake mbalimbali nchini na kuwainua zaidi.

Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni ya TDL, wazalishaji wa Konyagi ambao ni wadhamini wa #MwanamkeKinara Doreen Tumurebire, ameipongeza kampeni hiyo na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano zaidi katika kampeni hiyo, huku mwakilishi wa East Africa Television Limited, Nancy Mwanyika, akiwataka wafanyabiashara na wamiliki wa makampuni hasa zinazozalisha bidhaa za wanawake kuchangamkia fursa na kutangaza katika vipindi vya #DADAZ na #MamaMia.

Kilele cha kampeni ya #MwanamkeKinara kitafanyika Machi 19 mwaka huu, huku wanawake mbalimbali wakitarajiwa kushiriki katika kuhitimisha kampeni hiyo.