
Kazi hizo ni pamoja na kuteka maji na kusenya kuni, ikilinganishwa na wavulana , imesema ripoti ya shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF iliyotolewa, kabla ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike itakayoadhimishwa Jumanne ijayo Oktoba 11.
Ripoti inaonyesha kwamba tofauti hiyo huanza mapema na mara nyingi kazi zinazofanywa na mtoto wa kike hazionekani na hazithaminiwi.
Maeneo yaliyoathirika zaidi ni pamoja na Somalia, Burkina Faso na Yemen, huku utafiti ukitaja kuwa wasichana wa miaka 10 na 14 Kusini mwa Asia, Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini hutumia muda mara mbili kufanya kazi za nyumbani kuliko wavulana.