Jumanne , 14th Feb , 2023

Wazee mkoani Lindi wameitaka serikali kupitisha sheria ya mzazi kumshtaki mtoto wake endapo atamtelekeza mzazi wake bila kumpatia msaada wowote. 

Wazee mkoani Lindi

Wazee hao wamesema katika nyakati zao za uzee wanahitaji usimamizi na msaada kwa kuwa hawana nguvu tena ya kuhangaika kama zamani.

Hayo yamezungumzwa katika kikao cha baraza la wazee mkoani Lindi ambapo Afisa Ustawi wa Jamii mkoani humo Stella Starford amesisitiza kuwa, kwa tamaduni za Kiafrika jitihada za mzazi kumtunza mtoto hazitakiwi kupotea bure, ni wajibu pia wa watoto kuwalea wazazi wao. 

Aidha hoja ya kujenga vituo kwan ajili ya kulea wazee imeonekana sio nzuri kwani wazazi wana watoto wanaoweza kuwamudu hivyo kumuweka mzazi kituoni ni jambo la aibu na huashiria thabiti kuwa wazee wameshindwa kusaidika.