Jumatano , 25th Jan , 2023

Mtandao wa Wanawake, Katiba na Uongozi nchini umeiomba serikali kufanya marekebisho ya rasimu ya mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili kwa wanawake, watoto na wanaume wa mwaka 2023-2027 kwa kuondoa neno wanaume katika rasimu hiyo.

Wanawake wanaounda Mtandao wa Wanawake Tanzania, wakiongozwa na Dkt Ave Maria Semakafu (Kushoto) na Rebeca Gyumi, wa pili kutoka kushoto

Kwani kufuatia takwimu za matukio ya ukatili kwa sasa kuonekana asilimia kubwa yamekuwa yakisababishwa na kundi hilo la wanaume .

Mtandao huo umepinga uwepo wa kundi la wanaume katika rasimu hiyo kufuatia takwimu za sasa kuonesha asilimia kubwa ya wahanga wa matukio ya ukatili ni akina mama na watoto na si wanaume kama inavyojumuishwa katika mpango huo.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana Initiative Rebeca Gyumi, kwa pamoja wameiomba serikali kutekeleza makubaliano yaliyoafikiwa wakati wa uchukuaji maoni wakati wa mkutano wa wanajukwaa hilo na waandishi wa habari.

Kwa upande wake Dkt Ave Maria Semakafu pamoja na Dkt Rose Ruben ambaye ni Mkurugenzi wa TAMWA wamesema  kutokana na kukosekana na utafiti na ripoti za hali ya ukatili kwa wanaume serikali haina budi kutumia mpango kazi huo kwa ajili ya kusaidia kupunguza vitendo hivyo kwa makundi  ya wahanga wakubwa wa ukatili huku kwa baadhi ya wanaume  iwasaidie kupitia sehemu nyingine za kisheria