Jumapili , 30th Oct , 2022

Serikali kupitia kwa  Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa jamii na lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. James Kengia imewataka sasa wataalamu wa afya kwenda kuanzisha kliniki za magonjwa yasiyoambukiza katika vituo vyao vya kutolea huduma ili kubaini vyanzo vya magonjwa hayo katika

Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa jamii na lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. James Kengia

Dkt. Kengia amesema hayo wakati akifunga mafunzo ya magonjwa yasiyoambukiza yaliyoratibiwa na Wizara ya Afya, OR TAMISEMI pamoja na Wadau wa chama cha Kisukari Tanzania (TDA) kwa Watoa huduma (Madaktari, Wauguzi) pamoja na wakufunzi Jijini Dodoma.

"Tutakaporudi vituoni tuhakikishe tunaanzisha kliniki za magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa vituo ambavyo havina na kuboresha kliniki hizo kwa maeneo ambayo zipo tayari, kazi hii ifanywe kwa ushirikiano na wauguzi ambao pia nimepata taarifa wapo waliopatiwa mafunzo haya." Amesema.

Sambamba na hilo, amewataka kuandaa Mikakati shirikishi na Mipango shirikishi na jumuishi ya kutekeleza Afua mbalimbali za kukinga na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza, Afya ya akili na ajali katika maeneo yao ya kutolea huduma.