Ijumaa , 7th Oct , 2016

Watalii wanaotoka nchini Kenya kwenda nchini Afrika Kusini wameongezeka kwa asilimia 6.7 ndani ya miezi saba ya mwaka huu.

Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Sekta ya Utalii Afrika Kusini, Bi. Evelyn Mahlaba (Mwenye nywele Nyeupe) akizungumza na Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.

Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Sekta ya Utalii Afrika Kusini, Bi. Evelyn Mahlaba, amesema watalii wanaotoka Kenya kutembelea Afrika Kusini kutokea Januari hadi Julai mwaka huu wamefikia 15,719 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Bi. Mahlaba amesema kuwa wengi wa watalii kutoka Kenya wanaotembelea Afrika Kusini huenda kwa ajili ya kuponda raha, wanaosafiri kibiashara pamoja na wale wanaoenda mapumzikoni.