Jumanne , 11th Oct , 2022

Watu watano wakiwemo wawili wa familia moja ambao walikuwa wakielekea msibani wilayani Kyela, wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyohusisha gari ndogo aina ya Coaster na basi la kampuni ya Kyela Express kugongana uso kwa uso eneo la Kiwira wilayani Rungwe.

Magari yaliyopata ajali na kusababisha vifo vya watu watano

Mganga Mkuu wa Hosptali ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, Diodes Ngaiza, amethibitisha vifo vya watu watano na majeruhi 31  na kwamba baadhi wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Igogwe na wengine Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya.

Miongoni mwa waliofariki dunia ni pamoja na Enele Mwakalobo na Francis Mwakalobo ambao walikuwa wakielekea kwenye msiba wa ndugu yao Esther Mwakalobo.