Jumatano , 15th Feb , 2023

Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Humfrey Polepole amewahimiza watanzania kuchangamkia fursa mbalimbali za kibiashara zilizopo nchini Malawi, huku akiahidi Ubalozi huo utaendelea kuwasaidia kupata masoko sahihi.

Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Humfrey Polepole akizungumza katika kipindi cha Supa Breakfast kinachorushwa Jumatatu hadi Ijumaa saa 11 alfajiri hadi saa 3 Asubuhi East Africa Redio

Akizungumza wakati wa mahojiano katika kipindi cha Supa Breakfast kinachorushwa Jumatatu hadi Ijumaa saa 11 alfajiri hadi saa 3 Asubuhi East Africa Redio, Balozi Polepole amebainisha kuwa kwa kiasi kikubwa wananchi wa kipato cha chini na kipato cha kati wanategemea zaidi bidhaa kutoka Tanzania.

Aidha Balozi Polepole akatoa ufafanuzi kuhusu changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo madereva wa malori wakiwa nchini Malawi, akiwataka kutosita kumpigia ikiwa watapata changamoto yoyote wakiwa njiani.

Alipoulizwa kuhusu suala ya mikutano ya hadhara kuruhusiwa na kukuwa kwa demokrasia Tanzania, Balozi Polepole akabainisha kuwa sera bora za mambo ya ndani zimekuwa kivutio cha wawekezaji kuja kuwekeza nchini.