Jumatano , 29th Jul , 2015

Waziri wa maendeleo nyumba na makazi William Lukuvi amewataka wahusika wa benk ya wananchi MUCOBA kuwafikia wakulima waliopo vijijini ili kuwa fursa ya kujiunga na utoaji wa hisa.

Waziri wa maendeleo nyumba na makazi William Lukuvi

Mh Lukuvi amesema kuwa uchumi wa watu wadogowadogo kama wakulima ndio chanzo cha kukuza uchumi wa benk hivyo kunaumuhimu wa kuwafikia.

Amewataka pia wananchi kuwa na mazoea ya kununua hisa kwa wingi ili kuweza kuongeza kipato cha nchi na familia kwa ujumla kutokana na kuwa kununua hisa kunasaidia kukuza mtaji wa biashara .

Mkuu wa mkoa wa Iringa amewaagiza wafanyakazi wa wilaya zote za mkoa wa Iringa kununua hisa katika benki ya wananchi MUCOBA kulingana na uwezo walionao.

Benki ya wananchi MUCOBA inajumla ya wanahisa elfu nne na ishirini kwa kila benk.