Jumatatu , 29th Jun , 2015

Mkuu wa Mkoa wa Mara Kapteni Mstaafu Asery Msangi ametoa miezi mitano kwa uongozi wa Manispaa ya Musoma mkoani humo, kuhakikisha unaongeza wanachama elfu tatu katika mfuko wa afya ya jamii CHF.

Mkuu wa Mkoa wa Mara Kapteni Mstaafu Asery Msangi.

Msangi amesema kuwa serikali haitasita kuchukua hatua za kali zikiwemo za kuwafukuza kazi watendaji watakaoshindwa kusimamia agizo hilo.

Mkuu huyo wa mkoa wa mara ametoa agizo hilo wakati akizungumza wananchi, viongozi na watendaji mbalimbali wa manispaa ya musoma,

Amesema hatua ya viongozi hao kushindwa kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo wa afya ya jamii CHF imechangia vituo vingi kukosa fedha za kununulia dawa na vifaa tiba.

Hata hivyo kiongozi huyo wa Mkoa wa Mara ambaye anafanya ziara ya kukagua huduma na miuondombinu ya sekta ya afya, amegiza watendaji mkoani humo kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa uzazi wa mapango pamoja na kuchukua hatua kali katika kukomesha vitendo vya ukeketaji watoto wa kike