Alhamisi , 7th Jul , 2022

Takriban watoto 13 kusini mwa Ethiopia wamefariki kutokana na njaa wakati ukame na migogoro ikiendelea kukumba eneo hilo.

Mamlaka za eneo hilo zimesema huku Afisa mmoja kutoka wilaya ya Konso akithibitisha vifo hivyo.
Amesema kuwa kushindwa kustawi kwa mazao kuliendelea kuwasukuma wengi kutoka kwenye nyumba zao na mashamba yao. 

Afisa huyo amesema idadi ya watoto wenye utapiamlo katika wilaya hiyo inaongezeka, huku zaidi ya 240 kati yao wakilazwa hospitalini.

Eneo la Pembe ya Afrika linakabiliwa na ukame mbaya zaidi katika miongo kadhaa huku mashirika ya misaada yakisema kuwa watoto milioni saba walio chini ya umri wa miaka mitano wanakabiliwa na utapiamlo mkali. 
Kusini mwa Ethiopia ni moja ya maeneo yaliyoathiriwa sana na ukame ambao umewaacha watu milioni 18 katika eneo hilo bila chakula cha kutosha.