Hayo yamebainika mkoani Iringa wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Faustine Ndugulile, alipotembelea vikundi vya malezi kwa watoto katika kijiji cha Kising’a, kilichopo Wilaya ya Iringa mkoani humo.
Akitoa taarifa hiyo Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Saida Mgeni, amesema kuwa Mkoa huo unakabiliwa na matatizo mbalimbali na umekuwa ukiongoza katika masuala mabalimbali yasiyofaaa katika jamii, ikiwemo vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Kwa upande wake Naibu Waziri Dkt Ndugulile, amesema kuwa Serikali haijalala wala kufumbia macho suala la vitendo vya ukatili wa kijinsia, dhidi ya wanawake na watoto, bali inachukua hatua kali kwa wahusika wa vitendo hivyo wanapobainika.
"Mkiona wanajamii miongoni mwenu wanataka kumalizana katika kesi za vitendo vya ukatili wa kijinsia, toeni taarifa ili tukomeshe vitendo hivi visiendelee nchini" amesema Dkt Ndugulile.
