Jumatatu , 8th Apr , 2024

Watoto  nane wamefariki dunia katika matukio tofauti yaliyokotea mkoani Mbeya likiwemo tukio la watoto watatu wa familia moja walioliwa na Fisi katika kitongoji cha Gengeni kilichopo kata ya Kambikatoto, tarafa ya kipembawe wilayani Chunya mkoani Mbeya.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Abdi Isango

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya SACP Abdi Isango inaeleza kuwa tukio la kwanza la watoto kuliwa na fisi  limetopokea April 07, 2024 ambapo inadaiwa Fisi huyo alivamia nyumba ya Shigela Ngasa (45) mkazi wa Gengeni na kuwauwa kwa kuwang’ata watoto watatu wa familia hiyo ambao ni Samweli Shigela (05), Kasunzu Shigela  (03) na Ngasa Shigela mwaka 1

Aidha, katika tukio hilo mnyama huyo aliwajeruhi wazazi wa watoto hao ambao ni Shigela Ngasa (Baba) na mke wake aitwaye Limi Masanja (38) wote wakazi wa Gengeni na baada ya tukio hilo fisi huyo aliua kondoo wawili kisha akakimbia uelekeo wa hifadhi ya pori la akiba  Rungwa eneo la Kambikatoto.

Katika tukio lingine Mnamo Aprili 07, 2024 katika kitongoji cha Katagho kijiji cha Ngeleka, kata ya Makwale, tarafa ya Ntebela wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya, watoto watano wakiwemo mapacha wamefariki dunia wakati wanapatiwa matibabu katika zahanati ya Uhai Baptist baada ya kuzama ndani ya dimbwi la maji lililopo kwenye shamba la Kakao.

Watoto waliofariki katika tukio hilo wametambulika kwa majina ya rahel christopher mwaikale (5) mwanafunzi darasa la kwanza shule ya msingi ngeleka, carolina anosisye mwamkamba (6) mwanafunzi darasa la kwanza shule ya msingi

Makwale, Catherine Anosisye Mwamkamba (doto) (6) mwanafunzi darasa la kwanza shule ya msingi makwale, Lightness Ephraim Kakenda (5) mwanafunzi wa chekechea shule ya msingi Ngeleka na Kalebu Atufigwege Mwaikombe (5) mwanafunzi wa chekechea shule ya msingi Ngeleka.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa watoto hao walienda kuogelea kwenye dimbwi lililojaa maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha ndipo walizidiwa na maji na kuzama, walipiga kelele kuomba msaada wa kuokolewa na wananchi lakini tayari walikuwa katika hali mbaya.

Watoto hao walikimbizwa katika zahanati ya Uhai Baptist hata hivyo walifariki dunia wakiwa wanaendelea kupatiwa matibabu.