Jumanne , 11th Oct , 2022

Katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya mtoto wa kike, wasichana kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wameungana na kupaza sauti zao kwa pamoja kwa kuitaka serikali kuhakikisha inaondoa mifuko yote ya kisheria inayokwamisha upatikanaji wa elimu kwa mtoto wa kike hasa yule anayeishi kijijini

Watoto wa kike

Wakitoa tamko lao la pamoja hii leo Oktoba 11, 2022, wasichana hao wamesema mtoto wa kike amekuwa akiozeshwa kwa mwanaume mwenye umri mkubwa ambapo wapo wengine walioozeshwa kwa wanaume hao na hatimaye kuambukizwa virusi vya ukimwi  kwa sababu mwanaume husika alilipa mahari kubwa.

Aidha wasichana hao wamewaomba wazazi kuwa na lugha nzuri kwa watoto wao wa kike pale wanapowaomba fedha za kununulia taulo za kike wanapokuwa kwenye hedhi kwani wamebaini baadhi ya wazazi kuwatamkia watoto wao kwamba sasa wameshakuwa wakubwa hawezi kumhudumia kila kitu ikiwemo kumnunulia taulo hizo.