Watoto 10 wapoteza maisha baada ya shule kuungua

Jumatatu , 14th Sep , 2020

Shule ya Msingi Byamungu Islamic iliyoko Kata ya Itera wilayani Kyerwa mkoani Kagera, imeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Septemba 14, 2020.

Sehemu ya eneo la bweni lililoungua moto katika shule ya Byamungu Islamic

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya hiyo Rashid Mwaimu amesema kuwa watoto 10 wamethibitika kupoteza maisha.

Bweni hilo lilikuwa na wanafunzi 74.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, amewasili eneo la tukio, ambapo wakati akizungumza kwa njia ya simu amesema mbali na vifo hivyo pia kuna majeruhi saba, na kwamba ameunda tume itakayochunguza tukio hilo.

Sehemu ya eneo la bweni lililoungua moto katika shule ya Byamungu Islamic

Sikiliza sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera hapo chini