Watu wenye ulemavu waomba ujenzi wa vyoo mashuleni

Jumamosi , 5th Dec , 2020

Katika kuadhimisha siku ya walemavu duniani shirika la peace for people with disability limejikita katika kuanzisha kampeni ya ujenzi wa vyoo rafiki kwa watu wenye ulemavu hasa mashuleni ili kuwasaidia wanafunzi wenye matatizo mbalimbali ya viungo.

Watu wenye ulemavu wakihamasisha ujenzi wa vyoo rafiki mashuleni

Akizungumza na kurasa Mkurugenzi wa taasisi hiyo Sophia mbeyela amesema kwa sasa serikali imejitahidi kuingiza watoto wenye ulemavu mashuleni lakini kumekuwa na changamoto ya vyoo hali inayowapa shida wanafunzi hao wakiwa shuleni.

Naye mmoja wa wazazi Agnes Kaguo Mbeyela ametoa wito kwa Serikali kuhakikisha wanaweka utaratibu wa kuwatambua watoto wenye ulemavu katika kila Kaya ili kuweza kuwapatia msaada badala ya kuwaweka barabarani kuombaomba.