
Kesi hiyo iliyo mbele ya Jaji Projest Lugazia, imedaiwa kuwa washtakiwa wanakabiliwa na kosa la mauaji ya polisi na mafanyakazi wa NMB tawi la Wami Morogoro na kuiba kiasi cha shilingi milioni 150.
Hata hivyo , upande wa mashtaka katika kesi hiyo (Jamhuri), umewaachia huru washitakiwa wawili Jackson Issawangu na Musa Mustafa kutokana na kutokuwa na mashtaka ya kujibu kuhusika na kesi hiyo.
Mnamo Aprili 20, 2006, watuhumiwa hao 16 katika eneo la Ubungo mataa, wanadaiwa kumuua kwa makusudi askari Konstebo Abdallah Marwa na mfanyakazi wa NMB Tawi la Wami Morogoro, Ernest Manyoni, Mbali kufanya mauaji, pia walipora pesa mali ya benki kiasi cha Sh150milioni.