Waziri aliyetumbuliwa na JPM atoa maelekezo

Jumatano , 12th Jun , 2019

Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Joseph George Kakunda, amekabidhi ofisi za Wizara hiyo kwa Waziri mpya Mh. Innocent Bashungwa, jijini Dodoma leo Juni 12, 2019.

George Kakunda

Wakati wa kukabidhi, Kakunda amempa maelekezo ya kuzingatia waziri mpya awapo kwenye majukumu yake, ikiwemo kujua vizuri bajeti ya wizara yake pamoja na sheria na kanuni zinazomwongoza.

Kwa upande wake waziri mpya Innocent Bashungwa, amewaambia wafanyakazi wa wizara hiyo kuzingatia na kufanyia kazi maagizo ya Rais Ndugu Magufuli Jumapili hususani viwanda vilivyobinafisishwa.