Jumapili , 16th Aug , 2020

Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene, amevionya vyama vinavyofanya siasa zenye viashiria vya kuvuruga amani na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kudhibiti jambo hilo bila kujali ni chama kipi kimefanya ili harakati za uchaguzi zisisababishe baadhi ya Watanzania kupoteza maisha.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene.

Simbachawene ameyabainisha hayo akiwa mkoani Kigoma katika ziara yake ya kikazi, na kusema wanasiasa wasitumie wananchi kujitafutia umaarufu wa kisiasa na kuwa wana jukumu la kuhakikisha kila hatua wanayoifanya haileti madhara kwa wananchi.

Tazama video hapa chini