Jumatatu , 13th Mei , 2019

Wakurugenzi wa Halmashauri nchini wametakiwa kutotumia fedha za mfuko wa jimbo bila idhini ya mwenyekiti wa mfuko huo ambaye ni Mbunge.

Waziri Waitara.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo, Mei 13 na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waitara wakati akijibu swali la Mbunge wa Konde, Khatibu Said Haji (CUF), ambaye alitaka kujua kuhusu umuhimu wa serikali kuongeza viwango vya fedha ili kuleta ufanisi.

"Wakurugenzi wa halmshauri nchini hawaruhusiwi kutumia fedha za mfuko wa jimbo bila idhini ya mwenyekiti wake ambaye ndio Mbunge wa jimbo husika", amesema Waitara.

Aidha, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye ulemavu, Jenista Mhagama, amesema serikali itatoa waraka mpya kuhusiana na fedha hizo ili kuwakumbusha wakurugenzi kwamba hawana mamlaka na fedha hizo.