Ijumaa , 25th Sep , 2015

Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi celina Kombani amefariki dunia nchini India alikokuwa amelazwa kwa takirbani mwezi mmoja kwa ajili ya Matibabu.

Alieyekuwa Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi celina Kombani.

Taarifa iliyotolewa na jana Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah imeeleza kuwa Waziri Kombani alikuwa akusumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari na shinikizo la damu.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo wa Bunge amesema kuwa Kombani alikuwa akisumbuliwa na magonjwa hayo kwa muda mrefu na kwamba mwili wake utarejeshwa nchini hapo kesho kwa ajili ya mazishi.

Hadi kifo chake waziri Kombani alikuwa ni Mbunge anayemaliza muda wake katika jimbo la Ulanga Mashariki Mkoani Morogoro kwa tiketi ya CCM na pia ndiye alikuwa mgombea wa chama hicho katika jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu.