
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Ametoa agizo hilo leo alipotembelea ofisi za makao makuu ya NCAA, zilizoko wilayani Ngorongoro mkoa Arusha wakati akizungumza na watumishi wa mamlaka hiyo pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafugaji ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani hapa.
"Nina taarifa zenu kuwa mlimuhamisha kwa siri faru John kreta na kumpeleka V I P Grumet Serengeti Desemba 17, 2015 na mliahidiwa kupewa sh. milioni 200 ambapo mkapewa sh. milioni 100 kwa ahadi ya kumaliziwa sh. milioni 100 nyingine baadaye,".
“Naomba niletewe nyaraka zote zilizotumika kumuomba na kumuondoa faru huyo na barua zilizotumika kujadili suala la faru John. Nasikia amekufa naomba pembe ziletwe ofisini na iwapo itathibitika aliondoka bila ya kufuata taratibu wahusika wote watachukuliwa hatua kali za kisheria,”.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu apega marufuku tabia ya baadhi ya watumishi wa mamlaka hiyo ambao wanawakabidhi watoto kupeleka ng’ombe wao ndani ya kreta. “ Watumishi wa Ngorongoro ndiyo wanaopeleka ng’ombe ndani ya kreta na si wenyeji. Sasa marufuku na tutakayemkuta hatutakuwa na msamaha naye,”.
Amewataka watumishi hao kuhakikisha wanakuwa waadilifu na wanafanyakazi kwa kufuata misingi ya kiutumishi na kuacha tabia za kuendekeza rushwa na wizi.