Waziri Mkuu wa Uingereze aliyejiuzulu Liz Truss,
Wakati akijiuluzu Truss amesema kwamba aliingia madarakani wakati ambao Taifa hilo likiwa kwenye machafuko makubwa kiuchumi na kimataifa.
Truss amesema kwamba alikutana na Mwenyekiti wa Kamati ya 1922 Sir Graham Brady, na kukubaliana kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi ndani ya wiki ijayo na kwamba yeye atasalia kuwa Waziri Mkuu hadi pale mrithi wake atakapopatikana.
Liz Truss amekuwa ofisini kwa siku 45 pekee, muda mfupi zaidi wa Waziri Mkuu yeyote wa Uingereza, Waziri Mkuu wa pili aliyehudumu kwa muda mfupi zaidi alikuwa George Canning, ambaye alihudumu kwa siku 119.